“Nitarejea” - Diamond Platnumz

Nitarejea - Diamond Platnumz

➧Diamond Platnumz

Plays : 144,750
Downloads : 229,530
Album (All Songs) :

Like us on Facebook:

“Nitarejea” Lyrics

Vipi mizigo umeshaweka tayari
Sijechelewa kaja achwa na gari
Basi jikaze usilie mpenzi
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi

Zile taabu na njaa msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma, sema ntafanya nini na pesa sina
nakuonea na huruma, bora niende mjini kusaka tumaa

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Wanajua kwamba nafsi na roho vitakuwa na wasiwasi
ukumbuke na moyo utajawa na simanzi
ntakapokuwa nakwenda shambani afu niko peke yangu honey
ntapokuja kuwa na majirani ntaumia aaah
pale napotoka kisimani ama nipo na kuni kichwani
sina wakunitua nyumbani ntaliaa

maneno yako yananfanya nakosa raha na mawazo
hata mwenzako sijawahi kufika dar huu ndo mwanzo
vile nakwenda na sijui pa kukaaa wala mavazi ooh
we niombee niepushwe na balaa na maradhi ooh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea
nawe usichoke kuvumilia na kila siku kuniombea

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
usisahau kama mkeo na wana, umetuacha na dhiki
vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

Unapokwenda kama ukifika salama, utukumbuke na sisi
Kumbuka mkeo na wana nyumbani, umetuacha na dhiki ooh
vile usijali ila naomba chunga sana, ogopa na marafiki
wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama, waambie sidanganyiki

ntarejea mama
niombee nirude salama
ohhh watoto wadanganye
ihh, ohh

Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejeanitarejea(nitarejea mama)
wadanganye na vibagia, waambie pipi ntawaletea
Kama watoto wakinililia waambie kesho nitarejea(nitarejea mama)
nawe usichoke kuvumilia, na kila siku kuniombea

Like Diamond Platnumz's “Nitarejea”? leave A Comment

This Week's Most Popular